• HABARI MPYA

  Monday, December 14, 2015

  TFF YAWATOLEA UVIVU SIMBA SC, YAWAAMBIA; "ACHENI MAMBO YA KIENYEJI"

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitaka klabu zote nchini, kuanzia za Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes na Ligi Daraja la Pili kuheshimu utaratibu uliowekwa wa usajili na utekelezaji wake.
  Taarifa ya TFF inakuja siku mbili baada ya Simba SC kulalamikiwa wachezaji wake iliyowasajili katika dirisha dogo kutoruhusiwa kucheza.
  Hao ni beki Novat Makunga na washambuliaji, Brian Majwega, Paul Kiongera na Hajji Ugando, ambao Simba SC ilishindwa kuwatumia Jumamosi dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Brian Majwega amesajiliwa Simba SC, lakini atalazimika kusubiri kwa wiki moja kabla ya kuanza kucheza

  Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba klabu zinapaswa kuzingatia kalenda za mwaka za usajili ambazo ni Dirisha Kubwa la Usajili  (Juni 15 – Agosti 20) na Dirisha Dogo la Usajili (Novemba 15 – Disemba 15).
  Amesema baada ya usajili, hufuatia kipindi cha pingamizi ambacho kuchukua wiki moja, kisha Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF kupitia mapingamizi hayo na kupitisha usajili wa wachezaji wote waliosajiliwa.
  "Kipindi cha usajili wa dirisha dogo ulifunguliwa Novemba 15 na utafungwa kesho Disemba 15, kipindi hichi hutumika kwa ajili ya uhamisho, kutangaza wachezaji wanaoachwa kwa mujibu wa kanuni, kutangaza wachezaji waliositishiwa mikataba, na kipindi cha pingamizi Disemba 16 – 22, na kuthibitisha usajili Disemba 23, mwaka huu," amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAWATOLEA UVIVU SIMBA SC, YAWAAMBIA; "ACHENI MAMBO YA KIENYEJI" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top