• HABARI MPYA

    Sunday, December 13, 2015

    ARSENAL YAREJEA KILELENI LIGI KUU YA ENGLAND BAADA YA KUIPIGA 2-0 ASTON VILLA

    MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND
    Leo; Desemba 13, 2015  
    Aston Villa 0 - 2 Arsenal
    Jana; Desemba 12, 2015  
    Bournemouth 2 - 1 Manchester United
    Crystal Palace 1 - 0 Southampton
    Sunderland 0 - 1 Watford
    Manchester City 2 - 1 Swansea City
    West Ham United 0 - 0 Stoke City
    Norwich City 1 - 1 Everton
    Aaron Ramsey (katikati) akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la pili dhidi ya Aston Villa leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    TIMU ya Arsenal imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 jioni ya leo dhidi ya wenyeji Aston Villa Uwanja wa Villa Park.
    Ushindi huo, unaifanya The Gunners ifikishe pointi 33 baada ya kucheza mechi 16, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 32, sawa na Leicester City wakati Manchester United sasa ni ya nne kwa pointi zake 29.
    Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Olivier Giroud kwa penalti ya utata dakika ya nane baada ya The Walcott kuonekana ameangushwa na lingine Aaron Ramsey dakika ya 38.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAREJEA KILELENI LIGI KUU YA ENGLAND BAADA YA KUIPIGA 2-0 ASTON VILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top