• HABARI MPYA

    Tuesday, September 01, 2015

    SIMBA NA YANGA ZAKABIDHIWA 'SILAHA ZA KAZI' TAYARI KWA VUMBI LA LIGI KUU BARA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BIA ya Kilimanjaro Premium Lager inayodhamini vilabu vikongwe vya Simba na Yanga imekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya milioni 70 kwa vilabu hivyo vitakavyotumika katika msimu wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza Septemba 12 mwaka huu.
    Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli Jijini Dar es Salaam jana.
    Vifaa hivyo ni pamoja na pamoja na jezi za mechi seti mbili kwa kila klabu, jezi za mazoezi, casual wear, mipira, sheen guard, viatu vya kuchezea mechi, viatu vya mazoezi,soksi, gloves za makipa na mavazi ya mabenchi ya ufundi.

    Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli (wa pili kushoto) akiwa na kaimu Katibu Mkuu wa Simba, Collin Frisch Premium (kulia), Meneja Msaidizi wa Kilimanjaro Premium Lager Silvanus Mazula (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko wa Klabu ya Yanga Omar Kaya wakati wa kukabidhi vifaa kwa vilabu hivyo Jijini Dar es Salaam tayari kwa msimu ujao wa Ligi huu. Kilimanjaro Premium Lager ndio mdhamini mkuu wa Simba na Yanga.

    Akikabidhi, Pamela alisema ni matumaini yake kuwa vilabu vyote viwili vitatunza vifaa vizuri na wachezaji watatumia vifaa vinavyohitajika katika sehemu husika. “Mchezaji hategemewi kwa mfano kusafiri na malapa au mavazi tofauti na yale yaliyotengwaa kwa kusafiria na yenye nembo ya mdhamini,” alisema.
    Alisema pamoja na kutoa vifaa kila mwanzo wa msimu, Kilimanjaro Premium Lager imeendelea kuhakikisha mishahara ya wachezaji inalipwa kwa wakati na pia ilinunulia vilabu vyote viwili mabasi ya kisasa ambayo vilabu vinatumia kusafiri na kwa masuala mengine yanayohusu wachezaji.
    Katika hatua nyingine alitoa pongezi kwa Simba na Yanga kwa kumaliza katika nafasi nzuri katika ligi kuu ya Voda msimu uliopita. Yanga waliibuka na ushindi huku Simba wakiwa wa tatu.
    “Sisi wadhamini tunapenda kuona ushindani ukiwa mkubwa mno na timu zote mbili zilenge kunyakua taji la ligi kuu na mataji mengine katika mashndan ya kimataifa.
    Alitoa changamoto kwa Simba ijitahidi msimu ujao iweze kushika nafasi ya kwanza au ya pili ili icheze mashindano ya kimataifa kama wenzao Yanga. Simba haijacheza mahindano haya wa misimu takriban mine sasa.
    “Timu zote zimesajili vizuri na hii imejidhihirishwa wazi kwani Simba hawajashindwa mechi hata moja tangu kufika kwa kocha mpya na Yanga pia wameshinda ngao ya hisani. Hii inadhihirisha kuwa msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa kwa hivyo timu zote mbili zianze kwa matokeo mazuri,” alisema meneja huyo.
    Alisema vilabu hivi vinapofanya vizuri ni fahari kwa mdhamini kwani anapata faida ya udhamini na kusisitiza kuwa Kilimanjaro Premium Lager ina lengo la kufikisha mpira wa Tanzania katika kilele cha mafanikio na ndio maana pia imejikita katika udhamini wa timu ya Taifa, Taifa Stars.
    Wa mujibu wa meneja huyo, msimu ujao unatarajiwa kuwa mgumu kwani kuna timu kama Azam, Mwadui, Ndanda , Mtibwa, Kagera ambazo ni tishio kwa hivyo ni lazima Simba na Yanga ziongeze juhudi ili kuendelea kubakia timu bora.
    Vifaa hivyo vilipokelewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Simba, Collin Frisch na Mkuu wa Idara ya Masoko wa Yanga, Omar Kaya ambao waliahidi kuvitumia vifaa hivyo vizuri na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZAKABIDHIWA 'SILAHA ZA KAZI' TAYARI KWA VUMBI LA LIGI KUU BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top