• HABARI MPYA

    Sunday, July 13, 2014

    CHELSEA YASAJILI WINGA WA BARCELONA MWENYE KIPAJI CHA HATARI

    KLABU ya Chelsea imemsajili kinda wa thamani ya juu kutoka akademi ya Barcelona, winga Josi Quintero.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ameposti picha kwenye akaunti yake ya Twitter akisaini Mkataba wa The Blues, akiambatanisha na maelezo kwamba 'furaha kusaini mkataba wangu wa kwanza wa mwanasoka wa kulipwa na klabu kubwa'.
    Dole tupu: Quintero akiwa amepozi na jezi za mazoezi za Chelsea 
    Talent: Josi Quintero puts pen to paper on his deal with Chelsea
    Kipaji: Josi Quintero akisaini Mkataba wa Chelsea

    Chelsea inafikiriwa kuzipiga bao klabu za Arsenal na Lyon ambazo nazo pia zilikuwa zinawania saini ya kinda huyo wa Ecuador, ambaye amekua akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu Januari. Mchezaji huyo alikuwa benchi wakati timu ya vijana ya Chelsea chini ya umri wa miaka 21 inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sutton United Jumamosi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YASAJILI WINGA WA BARCELONA MWENYE KIPAJI CHA HATARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top