• HABARI MPYA

    Sunday, July 13, 2014

    UHOLANZI YAONDOKA KOMBE LA DUNIA 2014 BILA KUFUNGWA HATA MECHI MOJA, YAIFUMUA 3-0 BRAZIL MECHI YA MSHINDI WA TATU


    Angalau: Nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie akishangilia na mchezaji mwenzake, Dirk Kuyt (juu) baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza kwa penalti katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji, nchini Brazil. Uholanzi ilishinda 3-0, mabao yake mengine yakifungwa na Daley Blind na 
    Georginio Wijnaldum. Uholanzi inaondoka na rekodi ya kutofungwa katika fainali za mwaka huu, ikishinda mechi zote na kutoa sare mbili, moja ya Robo Fainali waliyofuzu kwa matuta na nyingine ya Nusu Fainali waliyotolewa kwa matuta na Argentina. Fainali ni usiku wa Jumapili kati ya Ujerumani na Argentina. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UHOLANZI YAONDOKA KOMBE LA DUNIA 2014 BILA KUFUNGWA HATA MECHI MOJA, YAIFUMUA 3-0 BRAZIL MECHI YA MSHINDI WA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top