• HABARI MPYA

    Tuesday, July 22, 2014

    YANGA SC WAFUATA MARASHI YA PEMBA KABLA YA KWENDA KAGAME KUSAWAZISHA REKODI YA UFALME WA SIMBA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WAWAKILISHI wa Tanzania katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame, Yangs SC wanatarajiwa kuingia kambini Agosti 1, mwaka huu kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya 40.
    Yanga SC inayofundishwa Marcio Maximo anayesaidiwa Leonardo Neiva, wote Wabrazil na mzalendo Salvatoty Edward, imepangwa Kundi A katika Kombe la Kagame pamoja na wenyeji, Rayon Sport, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan Kusini na KMKM ya Zanzibar.
    Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de L’Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti, wakati Kundi C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El Merreikh ya Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
    Yanga watakwenda kuweka kambi Pemba kujiandaa na Kagame

    Timu 14 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo kuanzia Agosti 8 hadi 24 mwaka huu- jumla ya mechi 34 zikichezwa katika viwanja vya Amahoro na Nyamirambo, Kigali. 
    Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawadi.
    Wizara ya Michezo ya Rwanda na mashirika mengine yatadhamini michuano hiyo, itakayokwenda sambamba na maazimisho ya miaka 20 ya mauwaji ya kimbau.
    Televisheni ya kulipia ya Supersport ya Afrika Kusini ambao ni maswahiba wa muda mrefu wa CECAFA, ni miongoni mwa wadhamini pia na wataonyesha mechi zote za michuano hiyo moja kwa moja. 
    Yanga SC imetwaa mara tano taji la michuano hiyo, 1975 visiwani Zanzibar, 1993 na 1999 mjini Kampala, Uganda na mara mbili mfululizo pia 2011 na 2012 mjini Dar es Salaam na watakwenda Kigali mwezi ujao kujaribu kusawazisha rekodi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliotwaa mara sita, 1974, 1991 mjini Dar es Salaam, 1992 visiwani Zanzibar, 1995, 1996 mjiji Dar es Salaam na 2002 Zanzibar tena.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAFUATA MARASHI YA PEMBA KABLA YA KWENDA KAGAME KUSAWAZISHA REKODI YA UFALME WA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top