• HABARI MPYA

    Wednesday, July 30, 2014

    STARS WALIVYOONDOKA LEO DAR KWENDA AFRIKA KUSINI

    Kiungo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto anayecheza Al Markhiya ya Qatar, akiwaongoza wenzake jioni ya leo kuingia ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tayari kwa safari ya Afrika Kusini ambako timu hiyo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kwenda Msumbiji, kumenyana na wenyeji, Mambas katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco. Mchezo huo utafanyika mwishoni mwa wiki baada ya timu hizo kutoka sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki iliyopita
    Amri Kiemba akiingia ndani JNIA
    Kutoka kulia Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Simon Msuva
    Beki Aggrey Morris akiingia ndani ya JNIA
    Kocha Salum Mayanga kushoto akiwaongoza vijana wake
    Haroun Chanongo na Ramadhano Singano 'Messi' kulia
    Kocha Mart Nooij kulia akiwa na mfungaji wa mabao yote mawili ya Stars katika sare ya 2-2 na Msumbiji Dar es Salaam, Khamis Mcha 'Vialli'
    Kutoka kulia Shaaban Nditi, Deo Munishi 'Dida' na Mrisho Ngassa
    Kutoka kulia Himid Mao, John Bocco na Erato Nyoni
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS WALIVYOONDOKA LEO DAR KWENDA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top