• HABARI MPYA

    Tuesday, July 29, 2014

    KIONGERA AREJEA KENYA BILA KUSAINI SIMBA SC, MIDO LA BURUNDI KUTUA MSIMBAZI ALHAMISI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Paul Kiongera amerejea Nairobi, Kenya baada ya kukamilisha mazungumzo na uongozi wa klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam na kufikia makubaliano ya kusaini Mkataba. 
    Kiongera alilazimika kurejea haraka nyumbani kujiunga na timu ya taifa, Harambee Stars kwa ajili ya mechi ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika.
    Na uongozi wa Simba SC umempa tiketi ya kwenda Nairobi na kurudi Dar es Salaam- ili arejee baada ya kukamilisha majukumu yake ya kitaifa.
    Paul Kiongera amerejea Kenya bila kusaini Simba SC, lakini atarudi tena kuja kumalizana na Wekundu wa Msimbazi

    Aidha, kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Pierre Kwizera naye anatarajiwa kutua nchini usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Dar es Salaam kuja kusaini Mkataba.
    Kiungo huyo anayechezea klabu ya Afad Abidjan ya Ivory Coast alikuja nchini wiki iliyopita na kufanya mazungumzo na klabu hiyo na kufikia makubaliano ya kusaini Mkataba.
    Wachezaji hao wawili, iwapo watasaini Simba SC wataungana na wachezaji wengine watatu wa kigeni kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Hao ni mabeki Mkenya Donald Mosoti, Mganda Joseph Owino na mshambuliaji Amisi Tambwe wa Burundi. Kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic ameiagiza klabu hiyo kuhakikisha inasaini wachezaji hao ili kuimarisha kikosi kuelekea msimu ujao.
    Loga aliyetua Simba SC Desemba mwaka jana akitokea Gor Mahia ya Kenya, hakuwa na mwanzo mzuri Msimbazi baada ya timu hiyo kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
    Na baada ya kusaini Mkataba mpya mwezi huu, Mcroatia huyo ameahidi kuifanya Simba SC iwe timu bora msimu ujao- huku uongozi ukimuambia unataka ubingwa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIONGERA AREJEA KENYA BILA KUSAINI SIMBA SC, MIDO LA BURUNDI KUTUA MSIMBAZI ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top