• HABARI MPYA

    Friday, July 25, 2014

    RANIERI KOCHA MPYA UGIRIKI

    KOCHA wa zamani wa Chelsea, Claudio Ranieri ameteuliwa kuifundisha Ugiriki, Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema.
    Babu huyo Mtaliano mwenye umri wa miaka 62 anakwenda kurithi mikoba ya Fernando Santos, ambaye amemaliza mkataba wake baada ya Fainali za Kombe la Dunia, akiifikisha Ugiriki katika hatua ya 16 Bora.
    Ranieri amepewa mkataba wa miaka miwili na sasa atakuwa na jukumu la kuiwezesha Ugiriki kufuzu kwenye Fainali za Euro mwaka 2016.

    Changamoto mpya Ugiriki: Claudio Ranieri anatumai kuipeleka Ugiriki Euro 2016

    Mechi ya kwanza ya Ranieri itakuwa ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Ulaya dhidi ya Romania Septemba 7 na baadaye dhidi ya Ireland Kaskazini, Hungary, Finland na Visiwa vya Faroe alizopangwa nazo katika Kundi F.
    Mkongwe huyo amekuwa 'juu ya maws  tangu alipofukuzwa Monaco Mei baada ya kupiga kazi kwa misimu miwili. Ranieri alitengeneza jina lake nchini kwao aliposhinda taji la Coppa Italia akiwa na Fiorentina kabla ya kutimkia Valencia, ambako alitwaa Copa del Rey na Kombe la Intertoto.
    Akaenda kupiga kazi misimu minne Chelsea kabla ya kurejea kwa muda Valencia na kisha kupiga kazi Parma, Juventus, Roma na Inter Milan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RANIERI KOCHA MPYA UGIRIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top