• HABARI MPYA

    Tuesday, July 22, 2014

    VODACOM WADHAMINI WAKUU ZIARA YA MAGWIJI WA REAL MADRID NCHINI

    Na Samira Said, DAR ES SALAAM
    VODACOM Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara kikosi cha wachezaji nyota waliowahi kutamba Real Madrid ya Hispania, maarufu kama Real Madird Legends ambao watazuru nchini mwezi ujao.
    Meneja ziara ya magwiji wa Real Madrid, Dennis Ssebo amewaambia Waandishi wa Habari asubuhi ya leo katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam kwamba, mbali na Vodacom, wadhamini wengine wa ziara hiyo ni Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
    Meneja Ziara ya magwiji wa Real Madrid, Dennis Ssebo (katikati) ametaja wadhamini leo

    Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Madrid watakuja nchini Agosti 22.
    Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
    Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah.
    Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.
    Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VODACOM WADHAMINI WAKUU ZIARA YA MAGWIJI WA REAL MADRID NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top