• HABARI MPYA

    Friday, June 20, 2014

    RAIS MALINZI AWATAKA MAKOCHA WATUMIE UJUZI WAO

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewataka makocha wa mpira wa miguu wafanyie kazi kwa vitendo mafunzo wanayopata badala ya kuweka makabatini maarifa waliyopata.
    Akifunga rasmi mafunzo ya wiki mbili ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Dar es Salaam leo (Juni 20 mwaka huu), Rais Malinzi amewataka makocha hao kuwapa mafunzo ya awali (basic) walimu wa shule za msingi kwa vile TFF ina mpango wa kuhakikisha kila shule ya msingi nchini inapata mipira kumi kila mwaka.
    Tumieni ujuzi; Rais wa TFF Jama Malinzi amewapa somo makocha

     “Kila mwaka tutakuwa na mashindano ya kitaifa ya watoto wenye umri chini ya miaka 13 kuanzia mwaka huu. Hivyo ninyi makocha huko mnaporudi muwafundishe walimu wa shule za msingi mafunzo ya awali ya ukocha,” alisema.
    Kozi iliyohudhuriwa na makocha 26 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ilikuwa chini ya Wakufunzi wa CAF, Honour Janza kutoka Zambia, na Sunday Kayuni na Salum Madadi wa Tanzania. Janza pia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ).
    Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Abdalla Mohammed Juma (Zanzibar), Abdul Banyai (Temeke), Abdul Nyumba (Temeke), Abdulmutik Haji (Zanzibar), Aley Mohammed (Zanzibar), Ali Vuai Shein (Zanzibar), Dennis Kitambi (Morogoro), Dismas Haonga (Ilala), Emmanuel Massawe (Shinyanga), Fikiri Elias (Arusha), Fulgence Novatus (Mwanza), Hababuu Ali Omar (Zanzibar), Juma Mgunda (Tanga) na Kidao Wilfred (Ilala).
    Wengine ni Maka Mwalwisi (Mbeya), Malale Hamsini Keya (Zanzibar), Mecky Maxime (Morogoro), Mohammed Tajdin (Temeke), Mussa Furutuni (Dodoma), Nassor Salum Mohamed (Zanzibar), Peter Mhina (Ruvuma), Said Mohamed Abdulla (Zanzibar), Salim Makame (Zanzibar), Salum Ali Haji (Zanzibar), Sebastian Nkoma (Ilala) na Wane Mkisi (Dar es Salaam).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS MALINZI AWATAKA MAKOCHA WATUMIE UJUZI WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top