• HABARI MPYA

    Saturday, June 21, 2014

    YABAINIKA, BABU ALIAHIRISHA KWENDA KUTIBIWA SARATANI ILI KUMPONYA SUAREZ AIANGAMIZE ENGLAND

    MCHUA misuli wa Luis Suarez aliahirisha kwenda kupatiwa matibabu ya saratani kuhakikisha mshambuliaji huyo wa Uruguay anakuwa fiti na kucheza dhidi ya England. 
    Walter Ferreira, mwenye umri wa miaka 63, alitarajiwa kwenda kufanyiwa tiba hiyo kabla ya Kombe la Dunia. Faida ya uamuzi wake wa kuahirisha zoezi hilo ilionekana Alhamisi wakati mabao mawili ya Suarez yalipoitupa nje ya Kombe la Dunia England.
    Shukrani: Suarez akishangilia bao la kwanza na Walter Ferreira
    Deadly: Suarez almost singlehandedly downed England
    Bao la kifo: Suarez akimtungua Joe Hart

    Suarez, ambaye alimkimbilia Ferreira baada ya kuifungia Uruguay bao la kwanza la kuongoza, amekuwa akihudumiwa na mchua misuli huyo kwa wiki kadhaa zilizopita. 
    Ferreira alisema: "Nawashukuru benchi la ufundi liliniamini na kunipa kazi ya kumhudumia Luis.’
      Committed to the cause: Ferreira put his own cancer treatment on hold to help Suarez
      Majukumu: Ferreira alisitisha kwenda kufanyiwa tiba ya saratani ili amhudumie Suarez

      Suarez alitoa shukrani zake kwa Ferreira kwa kumuwezesha kuwa fiti ndani ya muda na kucheza dhidi ya England, ambao amewarudisha nyumbani mapema.
      "Kuna mtu ambaye alijua kiasi gani nilihitaji msaada wake. Kama si yeye (Ferreira) hata hapa nisingekuwepo. Nililia sana na yeye, kwa sababu ulikuwa wakati mgumu kiasi hicho, na wa kuchaganyanya kwa sababu amejitoa mhanga kubaki na mimi kwa muda wote,"amesema Suarez.
      • Blogger Comments
      • Facebook Comments

      0 comments:

      Item Reviewed: YABAINIKA, BABU ALIAHIRISHA KWENDA KUTIBIWA SARATANI ILI KUMPONYA SUAREZ AIANGAMIZE ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
      Scroll to Top