• HABARI MPYA

    Wednesday, June 25, 2014

    SUAREZ AMEKWISHA, FIFA KUMPA ADHABU KALI

    MSHAMBULIAJI Luis Suarez anakabiliwa na adhabu kali baada ya nyota huyo wa Liverpool kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini began jana Uruguay ikishinda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Dunia nchini Brazil.
    Kwa mara ya tatu akifanya kosa la ajabu kihistoria, mchzaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alinaswa na kamera akimtia meno mchezaji mwenzake begani.
    Hata hivyo, baada ya mechi hodari huyo wa kufunga mabao alijitetea akisema: "Hayo mambo yanatokea ndani ya boksi. Tulikuwa tunapambana, kifua dhidi ya bega nami nikapata pigo jichoni,".
    Ona hapa: Chiellini akionyesha sehemu ambayo aling'atwa na meno na Suarez

    Chiellini kwa upande wake amesema: "Suarez amefanya hivyo na anaweza kuepuka adhabu kwa sababu FIFA inataka nyota wake wabaki katika Kombe la Dunia. Ningependa kuona wanatumia video ya ushahidi dhidi yake. Refa aliona alama ya kung'atwa, pia, lakini hakufanya lolote juu ya hili,".
    FIFA imesema itachunguza tukio hilo leo baada ya refa  wa Mexico, Marco Rodriguez kutona wakati linatokea.
    Bodi hiyo ya soka duniani hapana shaka itamchukulia hatua kali Suarez, ikizingatia makosa yake ya kihistoria ya utovu wa nidhamu.
    Wana nguvu ya kumfungia hadi miaka miwili kama wataona inastahili. Inaweza kuwa Suarez atafungiwa mecnhi kadhaa, ambazo zitamfanya awe amemaliza kucheza Kombe la Dunia mwaka huu, Uruguay ikiwa imefuzu 16 Bora baada ya kuitoa Italia.Hot water: Luis Suarez clutches his teeth after appearing to bite Giorgio Chiellini
    Maji moto: Luis Suarez akisafisha meno yake baada ya kumng'ata Giorgio Chiellini

    Picha za bega la beki Chiellini zinaoneysha dhahiri alama ya meno baada ya Mtaliano huyo kuteremsha jezi yake kuonyesha ushahidi wa tukio hilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AMEKWISHA, FIFA KUMPA ADHABU KALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top