• HABARI MPYA

    Saturday, June 28, 2014

    KIGOGO FIFA ABWAGA MANYANGA BAADA YA KUKERWA NA ADHABU YA SUAREZ, ADAI HAKUTENDEWA HAKI, NI SHINIKIZO LA WAINGEREZA

    KOCHA Oscar Tabarez amesme kwamba Luis Suarez amefanywa mbuzi wa kafara na FIFA wakati akizunguma na Waandishi wa Habari Maracana jioni ya jana.
    Tabarez alisoma taarifa aliyoandaa kwa dakika 13 akisema kwamba, presha ya vyombo vya habari Uingereza baada ya kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini Jumanne iliyopita ndiyo imeisukuma FIFA kumfungia kwa miezi minne.
    Kocha huyo wa Uruguay kisha mara moja akatangaza kujiuzulu wadhifa wake katika Kamati ya Ufundi wa FIFA na amemuambia Suarez kwamba anaungwa mkono na wananchi wake wa Uruguay.
    Amewaka: Kocha wa Uruguay amesema Luis Suarez amefanywa mbuzi wa kafara na FIFASupport: Luis Suarez holds his daughter as he waves to fans outside his home in Montevideo
    Sapoti: Luis Suarez akiwa ameba mwanawe wa kike wakati akiwapungia mkono mashabiki nje ya nyumbani kwake, Montevideo

    Tabarez amesema: "Mara nyingi unasahau kwamba, mbuzi wa kafara ni ambaye ana haki na haswa katika kesi mahsusi kama hii, mbali na makosa na faulo aliyocheza, ametoa mchango uwanjani. Ni mchango ambao unatolewa na wachezaji wakubwa duniani.
    "Tunafahamu itifaki na si kwa sababu ya wasifu wake, kwa sababu ya makosa, lakini ana upande mwingine naye. Huo ni ujumbe: Adhabu imezidi mno.  "Kama kocha na profesa, na mwalimu wa zamani, nawasilisha nadharia ya mbuzi ya kafara. Unajua nazungumzia nini, utoaji wa adhabu, kwa mtu ambaye amefanya kosa, si uhalifu.
    "Natumaini nina jibu, lakini kama watu wengi, ambao tu hawawezi kufanya maamuzi ya kinidhamu - mani ameshindsa? Nani ameshindwa? Nani amenufaika? Nani ameuawa? Nani ameula upande wake? 
    "Kwa moja ya maswali hayo, sitakupa jibu la mwisho, lakini nitatafuta majibu. Adhabu waliyotoa katika maamuzi yao, inatia shaka. Baada ya tukio la Suarez na Chiellini tumeona mengi yaliyoibuka.  
    "Tunatakiwa kutoa adhabu na vikwazo, lakini jambo moja la lazima ni kusikiliza kutoka kwa muhusika.’ 
    Tabarez aliikandia vikali Kamati ya Nidhamu ya FIFA baada ya kushindwa kumpa Suarez nafasi ya kujitetea baada ya tukio dhidi ya Chiellini.  
    Tooth ache: Suarez fell to the ground and held his teeth after the encounter with Chiellini
    Anasafisha meno: Suarez akiwa amejiangusha chini baada ya kumng'ata  Chiellini
    The incident: Suarez connects with Chiellini's shoulder in Uruguay's 1-0 win over Italy
    Tukio: Suarez akimng'ata Chiellini began katika mchezo ambao Uruguay iliifunga 1-0 Italia

    Kocha huyo wa Uruguay, anajiandaa kwa mchezo wa leo dhidi ya Colombia Uwanja wa Maracana, hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia amewataka wananchi wa nchi yake kupinga uamuzi huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIGOGO FIFA ABWAGA MANYANGA BAADA YA KUKERWA NA ADHABU YA SUAREZ, ADAI HAKUTENDEWA HAKI, NI SHINIKIZO LA WAINGEREZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top