• HABARI MPYA

    Saturday, June 21, 2014

    VAN PERSIE AMFAGILIA KINOMA ROONEY, AMTAJA MCHAWI WA SOKA YA ENGLAND NA KUWAPA SOMO LA MAANA FA

    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney hatakiwi kubeba lawama kwa England kutolewa mapema katika Kombe la Dunia, amesema Robin van Persie, ambaye ameishauri FA ya nchi hiyo kutazama msingi wake wa soka ya vijana.
    Van Persie amesema Rooney na England walicheza vizuri dhidi ya Uruguay kiasi cha kutosha kushinda na kusonga mbele, na akamfagilia mshambuliaji mwenzake wa Mancheser United, ambaye alishutumiwa vikali baada ya kipigo cha England katika mechi ya kwanza dhidi ya Italia.
    "Niliangalia sehemu kubwa ya mchezo dhidi ya Italia na mchezo wote dhidi ya Uruguay, na ninafikiri ni aibu. England ilicheza vizuri mno na hawakuwa na bahati kabisa. Wayne alipambana sana, alicheza vizuri sana na angeweza kufunga mabao manne, hivyo sifikiri ni wa kulaumiwa.
    Hastahili lawama: Wayne Rooney akishangilia bao lake la kwanza la England katika Kombe la Dunia Alhamisi
    A portent of doom: Wayne Rooney fails to nod home from a yard as Uruguay's defence panics
    Wayne Rooney alipambana sana dhidi ya Uruguay

      "Wayne ni mchezaji mkubwa. Nimesema hive mara nyingi, Wayne alikuwa sehemu ya sababu mimi kuja Manchester United. Sijawahi kujuta kusema hivyo, kwa sababu kwa kufanya nays mazoezi na kucheza nays ananioyesha ni mchezaji wa kiwango cha dunia.
      "Alipiga mpira wa adhabu vizuri mno, alipiga shuti zuri lililookolewa na kipa, alipiga kichwa kilichogonga mamba wa juu na akafunga bao. Si wa kulaumu, Alijitoa kwa kitu kwa ajili ya nchi yake. Ni haki kumshutumu sana yeye.
      "Alipoteza nafasi tatu za kufunga kwa inchi chache, na hiyo maana yake alikuwa katikati ya mstari wa kushinda na kushindwa, baina ya kurudi nyumbani na kusonga mbele.’
      Dynamic duo: Wayne Rooney (left) and Robin Van Persie (centre) have struck up a relationship at Man United
      Wawili hatari: Wayne Rooney (kushoto) na Robin Van Persie (katikati) wakiwa mazoezini Man United

      Na Van Persie anaamini FA inapaswa kutazama muundo wake makocha na kuwekeza zaidi katika maendeleo ya vijana, kama ilivyo kwa Uholanzi na nchi nyingine zinazoongoza Ulaya: "Sasa ni juu ya FA kuwa na mtazamo sahihi ili kuona England itaelekea wapi.
      "Ni muhimu sana kuwekeza kwenye soka yaw vijana, katika makocha wazuri na vifaa kwa ajili ya nyota chipukizi kucheza,"amesema.
      • Blogger Comments
      • Facebook Comments

      0 comments:

      Item Reviewed: VAN PERSIE AMFAGILIA KINOMA ROONEY, AMTAJA MCHAWI WA SOKA YA ENGLAND NA KUWAPA SOMO LA MAANA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
      Scroll to Top