• HABARI MPYA

    Sunday, June 22, 2014

    TFF YAPELKA MIKAKATI MIZITO BUNGENI KUINUA SOKA YA TANZANIA

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    UONGOZI wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukiongozwa na Jamal Malinzi jana (Juni 21 mwaka huu) mjini Dodoma umekutana na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Mtanda (Mbunge wa Mchunga).
    Katika kikao hicho TFF ilielezea mikakati yake ya maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Msumbiji.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi

    TFF iliiahidi Kamati ya Bunge kuwa itaendelea kuwa inafanya shughuli zake kwa karibu na Serikali na kamati hiyo ya Bunge.
    Katika kikao hicho, ujumbe wa benki ya CRDB ukiongozwa na Meneja wa Electronic Banking, Bw. Mangire Kibanda ulihudhuria ili kutoa ufafanuzi juu ya mradi wa kuuza tiketi za elektroniki, mradi ambao maandalizi yanaendelea vizuri.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAPELKA MIKAKATI MIZITO BUNGENI KUINUA SOKA YA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top