• HABARI MPYA

    Thursday, June 26, 2014

    SUAREZ AKIONA CHA MOTO, ATIMULIWA KOMBE LA DUNIA NA KUFUNGIWA MIEZI MINNE NA FAINI JUU

    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuondoa nyota  wa Uruguay, Luis Suarez kwenye michuano ya Kombe la Dunia na kufungiwa pia kucheza Ligi Kuu ya England hadi mwishoni mwa Oktoba.
    Kamati ya Nidhamu ya FIFA, baada ya kikao chake cha zakdi ya saa 10 usiku wa jana na leo asubuhi, imemfungia Suarez mechi tisa za mashindano za ya kimataifa na miezi minne jumla kutojihusisha kabisa na soka.
    Hiyo inafuatia mshambuliaji huyo kumng'ata began beki wa Itakia Giorgio Chiellini, Uruguay ikiibuka na ushindi ulioivusha hatua ya 16 Bora- hiyo ikiwa ni mara ya tatu kwa mchezaji huyo kufanya hivyo.
    Suarez atakosa mechi 13 za Liverpool ingawa haiwesi kuathiri mazungumzo yoyote ya kuuzwa na ametozwa faini ya Pauni 65,000.
    Amekiona cha moto: Nyota wa Uruguay, Luis Suarez ameadhibiwa na FIFA kwa kumng'ata beki wa Italia

    Rais wa Chama cha Soka Uruguay, Wilmar Valdez amethibitidha watakata rufaa kupinga adhabu ya Luis Suarez aliyopewa na FIFA.
    Wadhamini wa mshambuliaji huyo, adidas wan a mazungumzo ya dharula juu ya mustakabali wao kwa mchezaji huyo.
    Uruguay inajiadaa kwa rufaa, lakini wazi Suarez atakosa mchezo wa kesho wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Columbia Uwanja wa Maracana Stadium.

    MECHI ZA LIVERPOOL ATAKAZOKOSA SUAREZ

    Agosti 16: Liverpool v Southampton
    Agosti 23: Manchester City v Liverpool
    Agosti 30: Tottenham Hotspur v Liverpool
    Septemba 13: Liverpool v Aston Villa
    Septemba 16: Champions League matchday 1
    Septemba 20: West Ham United v Liverpool
    Septemba 27: Liverpool v Everton
    Septemba 30: Champions League matchday 2
    Oktoba 4: Liverpool v West Bromwich Albion
    Oktoba 18: Queens Park Rangers v Liverpool
    Oktoba 21: Champions League matchday 3
    Oktoba 25: Liverpool v Hull City
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AKIONA CHA MOTO, ATIMULIWA KOMBE LA DUNIA NA KUFUNGIWA MIEZI MINNE NA FAINI JUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top