• HABARI MPYA

  Saturday, December 08, 2018

  SIMBA SC KUSAFIRSHA MASHABIKI ZAMBIA KWENDA KUISHANGILIA TIMU MECHI NA NKANA FC JUMAMOSI MJINI KITWE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imeandaa utaratibu maalum wa kusafirisha mashabiki wake kwedna Zambai kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatu ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Nkana FC Jumamosi ijayo.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema leo katika taarifa yake kwa Waandishi wa Habari kwamba kila shabiki atatakiwa kulipa kiasi cha 130,000 kwa safari ya kwenda Kitwe nchini Zambia na kurudi Dar es Salaam.
  Hajji, mtoto wa mchezaji nyota wa zamani wa Yanga SC, Sunday Manara ‘Computer’ amesema kwamba gari ya mashabiki itaondoka Dar es Salaam mapema Alfajiri ya Alhamisi na kufika Kitwe Ijumaa jioni.

  Manara ametahadharisha kila anayetaka kusafiri ahakikishe pamoja na nauli kamili na fedha za kujikimu akiwa huko, anapaswa pia kuwa na hati ya kusafiria inayokidhi matakwa ya kisheria na Hati ya chanjo.
  “Mwisho wa kujiandikisha kwa anayehitaji ni siku ya Jumanne jioni na pia ufanyaji wa malipo na tunawaomba mfanye mawasiliano na ndugu Jacob Gamaly ambaye ni Msaidizi wa Msemaji wa klabu kwa namba zifuatazo 0659 929420,0766 051826.  Tunategemea sana nguvu ya mashabiki kule Kitwe ili tufanye vizuri na hatimaye kufuzu hatua za Makundi,” ,”amesema Hajji Manara.
  Simba SC imefika hatua hii baada ya kuitoa Mbabane Swallows ya eSwatini, zamani Swaziland kwa jumla ya mabao 8-1, ikishinda 4-1 Dar es Salaam na 4-0 Manzini, wakati Nkana FC imeitoa UD Songo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 3-1, ikishinda 2-1 mjini na 1-0 Kitwe.
  Mechi ya kwanza baina ya Nkana FC na Simba  itafanyika mjini Kitwe nchini Zambia Jumamosi ijayo na marudiano yatafuatia Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kati ya Desemba 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUSAFIRSHA MASHABIKI ZAMBIA KWENDA KUISHANGILIA TIMU MECHI NA NKANA FC JUMAMOSI MJINI KITWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top