• HABARI MPYA

  Saturday, December 08, 2018

  YANGA HATARINI KUMKOSA NA MAKAMBO KESHO MECHI NA BIASHARA UNITED…GARDIEL, YONDAN NA TSHISHIMBI WAREJEA KIKOSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC iko hatarini kumkosa mshambuliaji wake tegemeo, Heritier Makambo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kesho dhidi ya Biashara United Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mkongo Mwinyi Zahera amesema kwamba Makambo ameumia mazoezini leo, lakini Daktari wa timu, Dk. Edward Bavu anafanya jitihada ya kumponya maumivu ilinaweze kucheza kesho.
  Tayari Yanga SC itawakosa viungo washambuliaji tegemeo wa timu, Ibrahim Ajib na Mrisho Ngassa kwa pamoja wanatumikia adhabu za kadi. 
  Ajib anaweza kuwahi kurudi sababu adhabu yake ni kadi za njano, lakini Ngassa alitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa Tanzania Prisons, Laurian Mpalile mjini Mbeya.
  Yanga SC iko hatarini kumkosa mshambuliaji wake tegemeo, Heritier Makambo dhidi ya Biashara United kesho Uwanja wa Taifa 
   

  “Wachezaji Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngasa wao moja kwa moja hawatokuwa sehemu ya mchezo wa kesho, ila Heritier Makambo ana asilimia 50 kwenye kushiriki mchezo wa kesho baada ya kupata maumivu kwenye mazoezi ya leo,”amesema Zahera leo mjini Dar es Salaam.
  Hata hivyo, kocha huyo Msaidizi wa timu ya taifa ya DRC pia, Zahera amesema kwamba habari njema ni kurejea kwa mbaeki Gardiel Michael na Kelvin Yondani pamoja na kiungo Mkongo mwenzake, Papy Kabamba Tshishimbi.
  “Tumejiandaa vyema kuwakabili Biashara Unided, maana mara zote unapocheza na hizi timu ndogo amabazo zipo chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu zinakamia sana, hivyo tumejiandaa vyema kuwakabili,”amesema Zahera, kocha wa Septemba na Novemba msimu huu wa Ligi. 
  Papy Kabamba Tshishimbi (kulia) na Gardiel Michael (kushoto) wamerejea kikosini baada ya kupona maumivu yao

  Yanga SC inahitaji ushindi kesho kurejea kileleni mwa Ligi Kuu baada ya jana Azam FC kuichapa Mbao FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi 39 baada ya kucheza mechi 15, ikiizidi kwa pointi moja Yanga SC iliyocheza mechi 14, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 27 za mechi 12 ni ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA HATARINI KUMKOSA NA MAKAMBO KESHO MECHI NA BIASHARA UNITED…GARDIEL, YONDAN NA TSHISHIMBI WAREJEA KIKOSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top