• HABARI MPYA

  Tuesday, October 16, 2018

  UGANDA YATANGULIZA MGUU MMOJA CAMEROON 2019

  MABAO mawili ya Faruku Miya leo yameipa ushindi wa 2-0 wa ugenini Uganda, The Cranes dhidi ya wenyeji Lesotho 'Mamba' Uwanja wa Setsoto mjini Maseru Stadium.
  Ushindi huo unaifanya Uganda ifikishe pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na kuendelea kuongoza Kundi L katika mbio za kuwania tiketi ya kuchea Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 nchini Cameroon.
  Tanzania baada ya ushindi wa 2-0 pia leo dhidi ya Cape Verde mjini Dar es Salaam sasa inashika nafasi ya pili kwenye kundi L, wakati Lesotho yenye pointi inashika mkia. Cape Verde yenye pointi nne ni ya tatu.   
  Katika mchezo wa leo, Miya alifunga bao la kwanza dakika ya tano kwa shuti baada ya kazi nzuri ya Allan Kateregga na Emmanuel Okwi walioshirikiana kupeleka shambulizi upande wa kulia.
  Mshambuliaji huyo anayecheza Croatia, alicheza pamoja na nyota wa KCCA, Patrick Henry Kaddu alifunga bao la pili dakika ya 36 kwa shuti zuri la mpira wa adhabu baada ya Okwi kuchezewa rafu upande wa kushoto wa Uwanja.

  Uganda sasa wanahitaji sare tu katika mchezo wao ujao na Cape Verde Novemba 16 mjini Kampala ili kujihakikishia tiketi ya AFCON ya pili mfululizo mwakani, kabla ya kwenda kukamilisha mewchi za kundi hilo mkwa kumenyana na Tanzania Dar es Salaam Machi 22 mwakani.
  Tanzania ambayo ushindi wake wa leo umetokana na mabao ya winga wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Msuva na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta mechi ijayon itamenyana na Lesotho Novemba 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA YATANGULIZA MGUU MMOJA CAMEROON 2019 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top