• HABARI MPYA

  Wednesday, October 17, 2018

  MADAGASCAR, MISRI, TUNISIA NA SENEGAL ZA KWANZA KUFUZU AFCON

  TIMU ya taifa ya Madagascar anapotokea rais wa CAF, Ahmad imefuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Equatorial Guinea 1-0 nyumbani jana.
  na baadaye, Misri, Senegal na Tunisia wakafanikiwa kuungana na Madagascar pia kukamilisha timu tano, kati ya 24 zinazotarajiwa kwenda Cameroon, nyingine ni wenyeji, Simba Wasiofungika.
  Huku timu mbili zinafuzu kutoka kila kundi kati ya yote 12, Madagascar ilikuwa ina nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kuanza mechi zao za Kundi A kwa ushindi wa ugenini dhidi ya Sudan mwaka jana.

  Madagascar imefuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika

  Na pamoja na ushindi wa nyumbani na ugenini wa 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea siku tano zilizopita na bao pekee la Njiva Rakotoharimalala jana mjini Antananarivo mambo safi sasa.
  Senegal ilishinda 1-0 nchini Sudan, shukrani kwa mfungaji, Sidy Sarr katika mchezo ambao Simba wa Teranga walimkosa mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane aliyeumia dole gumba.
  Pamoja na kumkosa mshambuliaji wake nyota, Mohamed Salah ambaye ni majeruhi, lakini Misri ilishinda 2-0 ugenini dhidi ya Swatini, zamani Swaziland, na ushindi wa 2-1 wa Tunisia mjini Niger ulivihakikishia vigogo hivyo vya Kaskazini kmwa Afrika kufuzu kutoka Kundi J. 
  Mabao yote ya Tunisia yalifungwa na Firas Chawat akiichezea timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza.
  Uganda inahitaji pointi moja zaidi kujihakikishia tiketi ya Cameroon mwakabi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Lesotho ugenini jana na Guinea nayo ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu licha ya sare ya 1-1 na Rwanda jana.
  Nyota wa Liverpool, Naby Keita alitolewa baada ya kipindi cha kwanza kufuatia kuumia misuli.
  Ivory Coast bado wana kazi ya kufanya , kwani jana walilazimishwa sare ya 0-0 ugenini na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), lakini inapewa nafasi kubwa ya kufuzu kutoka Kundi H pamoja na Guinea.
  Pamoja na kumkosa mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, Gabon ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini mjini Juba, bao pekee la Andre Biyogo Poko.
  Vibonde Shelisheli walitoa sare ya 0-0 na na Afrika Kusini katika kisiwa hicho cha bahari ya Hindi, wakati mshambuliaji Odion Ighalo aliifungia mabao mawili Nigeria katika ushindi wa 3-2 mjini Sfax akitoka kupiga hat trick dhidi ya Libya mwishoni mwa wiki.
  Nigeria sasa inaongoza Kundi E kwa pointi zake tisa ikifuatiwa na Afrika Kusini pointi nane na Libya nne.
  Hata hivyo, Afrika Kusini wana michezo mgumu dhidi ya Nigeria nyumbani mwezi ujao na Libya ugenini mwezi Machi mwakani, hivyo wako hatarini kuzikosa fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MADAGASCAR, MISRI, TUNISIA NA SENEGAL ZA KWANZA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top