• HABARI MPYA

    Monday, October 15, 2018

    JUMA MAHADHI ‘BADO BADO’ SANA KUREJEA YANGA SC, AREJESHWA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Juma Mahadhi ataendelea kukosekana zaidi Yanga SC baada ya mwishoni mwa wiki kurejeshwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
    Ofisa Habari Msaidizi wa Yanga SC, Godlisten Anderdon ‘Chicharito’ amesema kwamba Mahadhi alilazimika kurejeshwa Muhimbili kwa matibabu zaidi kufuatia kuumia goti Agosti mwaka huu.
    Na baada ya matibabu hayo, Chicharito amesema kwamba Mahadhi amepewa wiki mbili za kuendelea kupumzika bila kufanya mazoezi kabla ya kurejea hospitali kufanyiwa uchunguzi mwingine. 

    Ikumbukwe kiungo huyo mshambuliaji, Juma Mahadhi aliumia Agosti 19 mwaka huu kwenye mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
    Katika mchezo huo, Yanga SC ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Deus Kaseke dakika ya 43 na Mkongo Heritier Makambo dakika ya 47, kabla ya Abderrahmane Meziane kuwafungia USM Alger dakika ya 53. 
    Na Mahadhi aliingia kipindi cha pili akitokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya kiungo Pius Buswita, lakini kwa bahati mbaya hakumaliza mchezo baada ya kuumia naye akampisha Ibrahim Ajib.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JUMA MAHADHI ‘BADO BADO’ SANA KUREJEA YANGA SC, AREJESHWA MUHIMBILI KWA MATIBABU ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top