• HABARI MPYA

  Tuesday, October 16, 2018

  DOMAYO NA PAUL PETER WATAKUWA NJE KWA MIEZI MIWILI AZAM FC BAADA YA KUUMIA TIMU ZA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NYOTA wawili wa Azam FC, kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Paul Peter watalazimika kuwa nje ya Uwanja kwa miezi miwili kila mmoja kutokana na maumivu yanayowakabili. 
  Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd amesema kwamba wawili hao ambao wapo Afrika Kusini kwa matibabu wameambiwa na na Dk Robert Nicholas wa huko kwamba wanahitaji miezi miwili ya mapumziko.
  Wawili hao waliongozana na Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ wiki iliyopita kwenda Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.
  Jaffar amesema kwamba wachezaji hao wamepatiwa matibabu mazuri na Daktari Robert Nicholas aliyeanza kwa kuwachukua vipimo kabla ya kuwatibu na anaamini watarejea wakiwa imara zaidi.
  Wakati Paul Peter aliumia akiicheza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes Aprili mwaka huu, Domayo anayejulikana kwa jina la utani ‘Chumvi’ aliumia jana kwenye mazoezi ya timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa ikijiandaa kwa mechi na Cape Verde.

  Frank Domayo (kulia) akiwa na Paul Peter watakuwa nje kwa miezi miwili kila mmoja
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DOMAYO NA PAUL PETER WATAKUWA NJE KWA MIEZI MIWILI AZAM FC BAADA YA KUUMIA TIMU ZA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top