• HABARI MPYA

  Sunday, October 14, 2018

  AMUNIKE AMUITA NYONI STARS KUCHUKUA NAFASI YA HASSAN KESSY AMBAYE HATACHEZA JUMANNE KWA SABABU YA KADI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI mkongwe wa Simba SC, Erasto Edward Nyoni anayeweza kucheza kama kiungo pia ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mchezo wa marudiano na Cape Verde Jumanne. 
  Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Papa wa Bluu Jumanne katika mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wakitoka kuchapwa mabao 3-0 na Cape Verde Ijumaa Uwanja wa Taifa mjini Praia.
  Na leo kocha Mkuu, Mnigeria Emmanuel Amunike amemuita Nyoni kwenda kuziba pengo la beki wa kulia wa Nkana FC ya Zambia, Hassan Kessy ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya jadi za njano.


  Edward Nyoni ameongezwa Taifa Stars kuelekea mchezo wa marudiano na Cape Verde Jumanne

  Mali, Boubou Traore, Drissa Kamory Niare na Baba Yomboliba, mabao ya Cape Verde yalifungwa na mshambuliaji wa klabu ya Partizan ya Ligi Kuu ya Serbia, Ricardo Jorge Pires Gomes na beki wa MOL Vidi FC ya Hungary Ianique dos Santos Tavares maarufu kama Stopira.
  Huo unakuwa mchezo wa tatu wa Taifa Stars katika kundi bila ushindi, baada ya awali kutoa sare za 1-1 na Lesotho Dar es Salaam na 0-0 na Uganda mjini Kampala na wa pili tu kwa kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike tangu aanze kazi Agosti.
  Mchezo mwingine wa kundi hilo jana, Uganda, The Cranes ilijiimarisha kileleni baada ya ushindi wa 3-0, mabao ya Emmanuel Okwi  anayechezea klabu ya Simba ya Tanzania aliyefunga mawili dakika za  11 na 63 na Faruku Miya wa Farouk Miya wa HNK Gorica ya Croatia kwa penalti dakika ya 36.
  Uganda sasa ina pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, ikishinda mbili na kutoa sare, sasa ikifuatiwa na Cape Verde pointi nne za mechi tatu pia, wakati Tanzania na Lesotho zina pointi mbili kila moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMUNIKE AMUITA NYONI STARS KUCHUKUA NAFASI YA HASSAN KESSY AMBAYE HATACHEZA JUMANNE KWA SABABU YA KADI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top