• HABARI MPYA

  Sunday, October 14, 2018

  KIUNGO CHIPUKIZI WA SINGIDA UNITED, ALLY NG’ANZI AENDA KUCHEZA SOKA YA KULIPWA JAMHURI YA CZECH

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa Singida United, Ally Hamisi Ng’azi anatarajiwa kuondoka usiku wa leo kwenda kujiunga na klabu ya MFK VySkov ya Daraja la Pili nchini Jamhuri ya Czech. 
  Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba uongozi wa klabu hiyo unamtakia safari njema na mafanikio mema mchezaji wao huyu, ukiamini atafika mbali katika safari yake ya mpira.
  Festo amesema Ng'anzi kupata timu hiyo ni jitihada za Singida United kuwatafutia wachezaji wa Tanzania nafasi ya kucheza soka kwenye timu mbalimbali barani Afrika na hata nje ya Africa, hivyo tunaamini kuna wachezaji wengine watapata timu siku si nyingi.
  Amesema wanaendelea kusisitiza nidhamu na kujitambua kwa wachezaji wao ili waelewe kwamba mpira ni ajira, hivyo wajitambue na wacheze kwa malengo.
  Ng’anzi ni miongoni mwa wachezaji walioaidia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kupata tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika Mei mwaka jana nchini Gabon kabla ya mwaka huu kupandishwa U20.
  Ally Ng’azi anatarajiwa kuondoka usiku wa leo kwenda kujiunga na klabu ya MFK VySkov ya Daraja la Pili nchini Jamhuri ya Czech. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO CHIPUKIZI WA SINGIDA UNITED, ALLY NG’ANZI AENDA KUCHEZA SOKA YA KULIPWA JAMHURI YA CZECH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top