• HABARI MPYA

  Friday, November 03, 2017

  ‘ULABU’ WAWAPONZA MACHAKU NA BUSUNGU WASIMAMISHWA LIPULI FC

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA 
  KLABU ya Lipuli ya Iringa imewasimamisha kwa muda usiojulikana wachezaji wake wawili maarufu, kiungo Salum Machaku na mshambuliaji Malimi Busungu kwa makosa ya utovu wa nidhamu.
  Taarifa ya Msemaji wa Lipuli FC, Clement Sanga, kwa vyombo vya Habari haijafafanua utovu wa nidhamu uliowafanya wawili hao wasimamishwe, lakini habari za ndani kutoka kwenye timu hiyo zinasema ni ulevi wa pombe, kiasi cha kuathiri utendaji wao kazini.
  “Wachezaji Malimi Busungu na Machaku Salum Machaku wamesimamishwa kwa muda kwa makosa ya kinidhamu na suala lao kwa sasa linafanyiwa kazi na Kamati ya Utendaji kwa ushirikiano na Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi,” imesema taarifa ya Sanga na kuongeza.
  Kiungo Salum Machaku (kushoto) amesimamishwa kwa utobu wa nidhamu Lipuli FC

  “Kwa sasa itoshe kusema wachezaji hao bado ni mali ya Lipuli FC na taarifa rasmi juu ya hatma yao itatolewa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji na Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kitakachofanyika Jumapili ya tarehe 5 ya mwezi huu,”.
  Machaku, mchezaji wa zamani wa Simba na Busungu aliyewahi kuchezea Yanga, mara kadhaa wamekutwa na kashfa za ulevi wa kupindukia kiasi cha kuwaponza hadi kuondolewa kwenye baadhi ya timu za awali.
  Pamoja na hayo, kocha wa Lipuli, Suleiman Matola bado ana imani kubwa na wakongwe hao licha ya uchakavu wa nidhamu yao na ndiye aliyezuia hatua kali zaidi kuchukuliwa na uongozi dhidi yao. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘ULABU’ WAWAPONZA MACHAKU NA BUSUNGU WASIMAMISHWA LIPULI FC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top