• HABARI MPYA

    Saturday, November 11, 2017

    SERIKALI YAMTEUA ABUBAKAR BAKHRESA KAMATI YA AFCON – U17

    Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM 
    WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amemteua Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhresa Group Limited, Abubakar Bakhresa kuwa Mjumbe wa Kamati ya watu 25 ya Maandalizi ya Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa Miaka 17 (AFCON U-17) zitakazofanyika Tanzania mwaka 2019.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe amesema Kamati hiyo itaongozwa nay eye mwenyewe kama Mwenyekiti, wakati Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu ni Dk. Henry Tandau. 
    Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhresa Group Limited, Abubakar Bakhresa (kulia) akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli

    Mwakyembe amesema ni heshima kubwa kwa Tanzania kupewa uenyeji wa mashindano hayo, hivyo ni muhimu kwa Serikali kwa kushirikiana na TFF kufanya maandalizi ya mapema kwa ajili ya michuano hiyo.
    Aliwataja wajumbe wengine kwenye Kamati hiyo kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura, Wakili Dk. Damas Ndumbaro, Dk. Francis Michael, Mohamed Dewji, Yusuph Omary, Ahmed Mgoyi, Khalid Dallah, Waziri wa Maliasiri na Utalii Mh. Khamis Kigwangala, Nassib Mbaga, Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah, Dk. Alan Kijazi wa TANAPA, Dk James ambaye ni Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na mipango, Dk Makakala Kamishna wa Uhamiaji, Fred Manoki, Lameck Nyambaya, William Erio, Kelvin Twisa, Ladislaus Matindi na Mama Devota Mdachi.
    Mwakyembe alisema mwaka 2019 si mbali hivyo ni lazima yafanyike maandalizi ya mapema na Kamati hiyo itakutana Jumamosi ijayo kwa ajili ya kupanga ratiba nyingine pamoja na kluchagua Kamati nyingine ndogondogo.
    “Jumamosi tutakutana tena kwa ajili ya kupanga mambo mengine na kuiteuwa kamati ndogondogo za kusaidiana kwa ajili ya suala hilo na kuweka sawa mikakati mingine,” alisema Mwakyembe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAMTEUA ABUBAKAR BAKHRESA KAMATI YA AFCON – U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top