• HABARI MPYA

  Saturday, November 11, 2017

  UWANJA WA TAIFA KUANZA KUTUMIKA TENA NOVEMBA 24

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM 
  UWANJA mkuu wa Taifa ambao ulikuwa katika matengenezo kwa takribani miezi mitatu, sasa umefunguliwa na kutarajiwa kuanza kutumika rasmi kuanzia Novemba 24 mwaka huu.
  Akizungumza wakati wa kukabidhiwa Uwanja huo leo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema kwamba, Uwanja ni mzuri na sasa unaonekana kukamilika kwani hata vile vipara vilivyokuwa vinaonekana awali vimepotea.
  Mwakyembe alisema, Serikali itakabidhiwa Uwanja huo rasmi na Kampuni ya SportPesa ndani ya siku 10 na hivyo kuiomba TFF kwa kushirikiana na bodi ya Ligi kupanga mechi moja ichezwe katika zoezi la uzinduzi na makabidhiano ya uwanja huo.
  “Uwanja umekamilika na leo nimeukagua na kuridhishwa na ukarabati mkubwa uliofanywa, wamenambia baada ya siku 10 utakuwa tayari hivyo nimewaomba TFF  kuangalia uwezekano wa kutafuta japo mechi moja ichezwe wakati wa ufunguzi Novemba 24,” alisema Mwakyembe.
  Aliongeza kuwa wapo vijana sita ambao wamepatiwa mafunzo ya utengenezaji wa Uwanja hivyo ameomba kuangaliwa kwa ajira zao ili waweze kutumika katika viwanja vingene vya mikoani.
  Mwakyembe alisema, kubwa linalotakiwa kwa sasa ni watanzani kwa ujumla kushirikiana katika kuutunza uwanja huo kwani gharama kubwa zimetumika katika ukarabati wake ambazo awali zilitajwa ni shilingi Bilioni 1.2 lakini ukimalizika kabisa ndiyo watajua gharama zote zilizotumika.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UWANJA WA TAIFA KUANZA KUTUMIKA TENA NOVEMBA 24 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top