• HABARI MPYA

    Saturday, November 04, 2017

    NI AL AHLY AU WYDAD CASABLANCA KUWA BINGWA AFRIKA LEO?

    BINGWA mpya wa soka anatarajiwa kupatikana leo wakati michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa itakapofikia tamati kwa mchezo wa marudiano wa fainali kati ya Wydad Athletic Club ya Morocco na Al Ahly ya Misri.
    Uwanja wa Mohamed V Complex uliopo mjini Casablanca wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 indigo utahodhi final hiyo ya pili leo. 
    Time hiss zilitoka are ya kufungana bro 1-1 katika mchezo wa kwanza wikiendi iliyopita mjini Alexandria, hivyo kuufanya mchezo wa marudiano leo uwe mgumu zaidi na wazi kwa timu zote.
    Wakitaka kuongeza mataji yao manane ya rekodi ya ubingwa wa michuano hiyo, Ahly wanajikuta kwenye nafasi ngumu, kwani wanatakiwa kufunga ugenini ili kufanikisha ndoto za kutwaa taji la tisa na la kwanza kwao tango mwaka 2013. 
    Kwa upande mwingine, sare ya bila mabao itawatosha Wydad kuonja taji la pili, baada ya taji lao la kwanza na pekee la michuano hiyo mwaka 1992.
    Ahly ilianza kupata bao mjini Alexandria kupitia kwa Moamen Zakaria dakika ya tatu, lakini Achraf Bencharki akasawazisha kwa kichwa dakika 13 baadaye. 
    Hiyo ilikuwa mechi ya tatu kwa timu hizo kukutana msimu huu, baada ya kill time kushinda 2-0 nyumbani kwake kwenye hatua ya makundi.
    Wydad wanacheza fainali ya tatu ya michuano hiyo mbili za awali wakishinda moja na kufungwa moja mwaka 2011, 
    Ahly wanacheza final ya 11, wakiwa wameonja vipigo viwili, 1983 na 2007.
    “Tunakwenda kucheza tofauti kabisa,” alisema kocha wa Wydad, Hussein Amoutta alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi ya kwanza.
    “Ndiyo, kuwabana kea sare Al Ahly genii ni matokeo mazuri, lakini hatujashinda chochote bado. Ni mechi tofauti kabisa sasa na tunapaswa kujiandaa vizuri tukipambana na timu yenye historia kubwa na uzoefu,” alisema. 
    Ammoutta mwenye umri wa miaka 48 awali aliiwezesha FUS Rabat kutwaa taji la Kombe la Shirikisho mwaka 2010 na anatarajia kuongeza taxi lingine ambalo ni la Ligi ya Mabingwa.
    Kea upande wake, kocha wa Ahly, Hossam El Badry ambaye pia aliwaongoza Mashetani Wekundu kutwaa taji hilo mwaka 2012 alikuwa mwenye matumaini wakati timu yake inakwenda Casablanca Jumatano. 
    “Tumepitia katika mazingira haya mara nyingi nyuma. Tunafahamu ugumu uliopo,” alisema El Badry alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Cairo kabla ya kwenda Morocco.
    “Tutajitolea kila kitakachohitajika ili kushinda taji hili, na ninawakubali vijana wangu wanaweza kufanya hivi,” alisema mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 57.
    Time zote zitawakosa baadhi ya wachezaji wake nyota ambao ni majeruhi kuelekea mchezo huu wa kuamua bingwa. 
    Winga mwenye kipaji wa Wydad, Mohamed Ounajem aliumua mguu kwenye mchezo wa kwanza, wakati wachezaji wawili wa Ahly, Mbeki wa kushoto Mtunisia, Ali Maaloul na kiungo, Hossam Ashour nao pia wako nje kwa maumivu ya nyonga.
    Bingwa wa michuano hiyo atapatiwa kitita cha doll za Kimarekani Milioni  2.5 na tiketi ya kucheza michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA mjini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.

    WASHINDI WA AWALI LIGI YA MABINGWA
    1965 Oryx Douala (Cameroon)
    1966 Stade d'Abidjan (Ivory Coast)
    1967 TP Mazembe (DRC) 
    1968 TP Mazembe (DRC)
    1969 Ismaily (Misri)
    1970 Asante Kotoko (Ghana)
    1971 Canon Yaounde (Cameroon)
    1972 Hafia Conakry (Guinea)
    1973 AS Vita Club (DRC)
    1974 CARA Brazzaville (Kongo)
    1975 Hafia Conakry (Guinea)
    1976 Mouloudia Alger (Algeria)
    1977 Hafia Conakry (Guinea)
    1978 Canon Yaounde (Cameroon)
    1979 Union Douala (Cameroon)
    1980 Canon Yaounde (Cameroon)
    1981 JS Kabylie (Algeria)
    1982 Al Ahly (Misri)
    1983 Asante Kotoko (Ghana)
    1984 Zamalek (Misri)
    1985 FAR Rabat (Morocco)
    1986 Zamalek (Misri)
    1987 Al Ahly (Misri)
    1988 Entente Setif (Algeria)
    1989 Raja Casablanca (Morocco)
    1990 JS Kabylie (Algeria)
    1991 Club Africain (Tunisia)
    1992 Wydad Casablanca (Morocco)
    1993 Zamalek (Misri) 
    1994 Esperance (Tunisia)
    1995 Orlando Pirates (Afrika Kusini)
    1996 Zamalek (Misri)
    1997 Raja Casablanca (Morocco)
    1998 ASEC Abidjan (Ivory Coast)
    1999 Raja Casablanca (Morocco) 
    2000 Hearts of Oak (Ghana)
    2001 Al Ahly (Misri)
    2002 Zamalek (Misri)
    2003 Enyimba (Nigeria)
    2004 Enyimba (Nigeria)
    2005 Al Ahly (Misri)
    2006 Al Ahly (Misri)
    2007 Etoile du Sahel (Tunisia)
    2008 Al Ahly (Misri)
    2009 TP Mazembe (DRC)
    2010 TP Mazembe (DRC)
    2011 Esperance (Tunisia)
    2012 Al Ahly (Misri)
    2013 Al Ahly (Misri)
    2014 ES Setif (Algeria)
    2015 TP Mazembe (DRC) 
    2016 Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI AL AHLY AU WYDAD CASABLANCA KUWA BINGWA AFRIKA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top