• HABARI MPYA

  Saturday, November 04, 2017

  NGASSA: SIMBA NI WAZURI, LAKINI TUTAJITAHIDI TAWAPIGA KESHO

  Na David Nyembe, MBEYA
  KIUNGO mshambuliaji mkongwe wa Mbeya City, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba mchezo dhidi ya Simba kesho utakuwa mgumu, lakini wamedhamiria kushinda.
  Mbeya City wanawakaribisha Simba SC katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kesho Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini hapa, Ngassa amesema watapigana washinde.
  “Simba ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri na wazoefu wenye hamasa zaidi, lakini hata sisi tuna timu nzuri na kesho tutajitahidi tushinde,”alisema Ngassa ambaye amewahi kuchezea Simba.
  Mrisho Ngassa amesema mchezo dhidi ya Simba kesho utakuwa mgumu, lakini wamedhamiria kushinda

  Mchezaji huyo wa zamani wa Free State Stars ya Afrika Kusini na Fanja ya Oman, amesema kwamba wanaijua Simba vizuri na waliiona ilipocheza na Yanga katika mchezo wao wa mwisho Oktoba 28 wakitoa sare ya 1-1 ndiyo maana anasema mchezo utakuwa mgumu.
  “Tuliwaana vizuri wakicheza na Yanga na baada ya hapo tukaanza kujipanga kutumia makosa yao tupate ushindi kesho. Tunaomba Mungu atusaidie tushinde,”amesema.
  Simba SC iliwasili Mbeya jana kwa ndege na leo imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wana Mbeya.   
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA: SIMBA NI WAZURI, LAKINI TUTAJITAHIDI TAWAPIGA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top