• HABARI MPYA

    Tuesday, November 07, 2017

    MOYES NDIYE KOCHA MPYA WA WEST HAM UNITED

    David Moyes atathibitishwa kuwa kocha mpya wa West Ham leo baada ya kufukuzwa kwa Slaven Bilic jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    REKODI YA SLAVEN BILIC WEST HAM UTD

    Mechi: 111 | Kushinda: 42 | Sare: 30 | Kufungwa: 39
    Asilimia ya ushindi: 37.84 
    KOCHA David Moyes atathibitishwa kuwa kocha mpya wa West Ham leo baada ya kufukuzwa kwa Slaven Bilic jana.
    Bilic alifukuzwa baada ya kikao na David Sullivan jana asubuhi na moja kwa moja, Moyes, aliyesafiri kutoka Qatar jana asubuhi kuja London anachukua nafasi.
    Moyes, mwenye umri wa miaka 54, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu, ambao utakuwa na kipengele cha kuondolewa mwishoni mwa msimu huu kama Mscotland huyo hatafanya vizuri.
    Bilic alifukuzwa West Ham United baada ya matokeo mabaya kutokana na The Hammers kushinda mechi mbili tu kati ya zote za Ligi Kuu ya England msimu wote na wanakwenda kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa wakiwa kwenye nafasi za mkiani, baada ya kufungwa 4-1 na Liverpool Jumamosi.
    Bilic alianza kazi West Ham mwaka 2015 na akaiwezesha kushika nafasi ya saba katika msimu wake wa kwanza.
    Lakini Mcroatia huyo akashindwa kurudia mafanikio ya msimu uliotangulia na West Ham ikaangukia katikati ya msimamo wa Ligi.
    Amefukuzwa pamoja na benchi lake lote la ufundi Uwanja wa London, akiwemo mchezaji wa zamani maarufu, Julian Dicks. West Ham itasafiri kwenda Uwanja wa Vicarage Road kumenyana na Watford baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOYES NDIYE KOCHA MPYA WA WEST HAM UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top