• HABARI MPYA

  Tuesday, November 14, 2017

  ALEX IWOBI AFUNGA MAWILI NIGERIA YAICHAPA ARGENTINA 4-2

  KIUNGO wa Arsenal, Alex Iwobi leo ameifungia mabao mawili timu yake ya taifa ya Nigeria ikiichapa 4-2 Argentina katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa FK Krasnodar mjini Krasnodar, Urusi.
  Iwobi alifunga bao la pili na la nne dakika za 52 na 73, wakati mabao mengine ya Super Eagles yalifungwa na Kelechi Iheanacho dakika ya 44 na  Brian Idowu dakika ya 54.
  Mabao ya Argentina ambayo ilimkosa nyota wake, Lionel Messi, yamefungwa na Ever Banega dakika ya 27 na Sergio Aguero dakika ya 36. 
  Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Iwobi akishangilia baada ya kuifungia Nigeria mabao mawili dhidi ya Argentina PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kikosi cha Argentina kilikuwa; Marchesin, Mascherano, Pezzella/Insua dk80, Otamendi, Perez, Banega, Lo Celso/Gomez, dk58, Pavon/Perotti, dk77, Di Maria/Rigoni, dk76, Dybala/Belluschi dk63 na Aguero/Benedetto dk46.Nigeria: Akpeyi/Uzoho dk46, Abdullahi/Ebuehi dk46, Troost-Ekong, Balogun/Omeruo dk61, Awaziem, Aina/Idowu dk46, Ndidi, Mikel, Ogu, Iheanacho/Musa dk70 na Iwobi/Kayode dk87.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALEX IWOBI AFUNGA MAWILI NIGERIA YAICHAPA ARGENTINA 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top