• HABARI MPYA

  Tuesday, November 08, 2016

  YANGA NA RUVU SHOOTING YAAHIRISHWA, SASA KUPIGWA ALHAMISI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga SC na Ruvu Shooting iliyokuwa ifanyike kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam sasa imesogezwa mbele hadi Alhamisi.
  Mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku moja kwa sababu Ruvu Shooting imechelewa kutoka Bukoba mkoani Kagera ambako Jumapili ilicheza na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limejiridhisha kuwa Ruvu Shooting imechelewa kuingia kituo cha Dar es Salaam, ndiyo maana mchezo dhidi ya Yanga umesogezwa mbele.
  Mechi nyingine za kesho zipo kama zilivyopangwa, Mwadui wakiikaribisha Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Prisons wakiikaribisha Simba SC Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA RUVU SHOOTING YAAHIRISHWA, SASA KUPIGWA ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top