• HABARI MPYA

  Friday, November 18, 2016

  NIGERIA WAINGIA NA MKWARA MZITO KUTETEA TAJI CAMEROON

  KOCHA wa Nigeria, Florence Omagbemi ameahidi timu yake kuendelea kucheza kwa kiwango cha juu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake mwaka (AWCON) 2016 nchini Cameroon.
  Nigeria itaanza kutetea taji lake la AWCON Jumamosi wakimenyana na Mali Uwanja wa Manispas ya Limbe na Omagbemi ameweka wazi kwamba "wanataka kutetea taji (la AWCON),".
  "Tunataka kudumisha kiwango chetu cha juu. Tunataka kutetea taji letu, kwa sababu hilo ndilo lengo letu Cameroon," alisema Omagbemi.
  Tayari Nahodha huyo wa zamani wa Nigeria amezitaja Cameroon na Ghana kama vikwazo vikuu kwa Super Falcons kutetea taji lao, lakini amesema pia timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo zinastahili kupewa heshima pia.
  Nigeria itamenyana na Ghana Novemba 23 katika mchezo wao wa pili wa Kundi B, kabla ya kumaliza na Kenya siku tatu baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIGERIA WAINGIA NA MKWARA MZITO KUTETEA TAJI CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top