• HABARI MPYA

  Monday, February 08, 2016

  VIPORO VYA AZAM VYAPATIWA TAREHE MWAFAKA, NI DHIDI YA PRISONS NA STAND

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI mbili za viporo za Azam FC dhidi ya Prisons na dhidi ya Mwadui FC zimepangiwa tarehe mpya.
  Azam FC itamenyana na Prisons Februari 24, mwaka huu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kabla ya kumenyana na Stand United Machi 16, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Lakini timu zote zitaendelea na ratiba iliyopo ya Ligi Kuu, Azam FC ikimenyana na wenyeji Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili, wakati Stand United wataikaribisha Simba SC Jumamosi mjini Shinyanga na Prisons wataifuata Mwadui FC Jumapili.
  Azam FC ilikuwa Zambia ambako imetwaa ubingwa wa michuano maalum

  Azam FC iliondolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu wiki mbili zilizopita ili iende kucheza michuano maalum ya kirafiki nchini Zambia.
  Katika michuano hiyo iliyoshirikisha pia timu za wenyeji, Zanaco FC na Zesco United pamoja na Chicken Inn ya Zimbabwe, Azam FC iliibuka bingwa.
  Baada ya kurejea nchini, Azam FC ilicheza mechi yake ya kwanza jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na kushinda 1-0 dhidi ya Mwadui FC, bao pekee la Kipre Herman Tchetche dakika ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIPORO VYA AZAM VYAPATIWA TAREHE MWAFAKA, NI DHIDI YA PRISONS NA STAND Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top