• HABARI MPYA

    Monday, February 08, 2016

    MECHI MBILI ZA YANGA LIGI KUU ZAAHIRISHWA, SASA IKITOKA MAURITIUS KUIVAA SIMBA FEB 20

    RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA…
    Februari 13, 2016
    Stand United Vs Simba SC
    Mgambo JKT Vs African Sports
    Mbeya City Vs Toto Africans
    Ndanda FC Vs Majimaji
    JKT Ruvu Vs Kagera Sugar
    Februari 14, 2016
    Mwadui FC Vs Prisons
    Coastal Union Vs Azam FC
    Yanga SC itaondoka Jumatano kwenda Mauritius kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MECHI mbili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania za klabu ya Yanga SC dhidi ya Mtibwa Sugar na dhidi ya African Sports zimefutwa na zitapangiwa tarehe nyingine.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba mechi hizo zimefutwa ili kupisha mechi mbili za Yanga SC za Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Yanga SC inatarajiwa kuondoka nchini Jumatano kwenda Mauritius kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Cercle de Joachim uliopangwa kuanza Saa 9:30 Alasiri kwa saa za huko Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe.
    Na timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye, Februari 27 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 
    Lakini mara tu baada ya mchezo wa kwanza na Joachim nchini Maurtius, Yanga itarejea kwenye Ligi Kuu kwa ajili ya mchezo na mahasimu wa jadi, Simba SC Februari 20, mwaka huu Uwanja wa Taifa. 
    Pamoja na hayo, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki, Stand United wakiikaribisha  Simba SC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT na African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mbeya City na Toto Africans Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Ndanda FC na Majimaji Uwanja wa Nangwanda SIjaona, Mtwara na JKT Ruvu na Kagera Sugar Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Februari 14 kutakuwa na mechi mbili, Mwadui FC dhidi ya Prisons Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga na Coastal Union na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI MBILI ZA YANGA LIGI KUU ZAAHIRISHWA, SASA IKITOKA MAURITIUS KUIVAA SIMBA FEB 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top