• HABARI MPYA

  Monday, February 08, 2016

  KAMUSOKO MCHEZAJI BORA LIGI KUU DESEMBA 2015

  KIUNGO Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko (pichani kushoto) amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Desemba 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga SC, Mrundi Amissi Tambwe).
  Kamusoko ameisaidia timu yake ya Yanga katika michezo iliyochezwa Desemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi huo wa mwisho wa mwaka.
  Kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMUSOKO MCHEZAJI BORA LIGI KUU DESEMBA 2015 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top