• HABARI MPYA

  Monday, February 08, 2016

  THOM 'RAMBO' ULIMWENGU AIZIDI KUPIGA MABAO MAZEMBE

  NYOTA ya Mtanzania Thomas Emmanuel Ulimwengu (pichani kulia) imeendelea kung'ara katika klabu ya Tout Puissant Mazembe baada ya leo kufunga bao katika ushindi wa 5-0 dhidi ya FC Lubumbashi kwenye mechi yab Ligi Kuu ya DRC.
  Ulimwengu, maarufu kwa jina la utani Rambo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alianza kwa kumsetia Roger Assale kufunga bao la kwanza dakika ya 16 Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
  Baadaye mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, akafunga bao lake mwenyewe dakika ya 23 kwa pasi ya Assale kabla ya Luyindama kufunga dakika ya 75 na  Rainford Kalaba mawili dakika ya 76 na 84 kuhitimisha sherehe za mabao ya Mazembe katika mchezo huo.
  Lakini Ulimwengu ambaye leo amefunga katika mechi ya pili mfululizo, alimpisha Kalaba dakika ya 63.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE baada ya mchezo huo, Ulimwengu amesema kwamba amefurahi kuendelea kufanya vizuri katika klabu hiyo chini ya kocha mpya, Mfaransa Hubert Velud, aliyerithi mikoba ya Patrice Carteron ambaye hakuongezewa Mkataba mapema Januari baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2013.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: THOM 'RAMBO' ULIMWENGU AIZIDI KUPIGA MABAO MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top