• HABARI MPYA

  Tuesday, February 09, 2016

  KART ZOUMA NJE MIEZI SITA, ATAKOSA HADI MICHUANO YA EURO 2016

  BEKI wa Chelsea, Kurt Zouma amekuwa mwenye masikitiko baada ya kuambiwa ataikosa sehemu yote iliyobaki ya msimu pamoja na michuano ya Euro 2016 kutokana na kuumia mguu.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa anatakiwa kuwa nje ya Uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia mguu katika mechi dhidi ya Manchester United Jumapili.
  Zouma atakwenda kufanyiwa upasuaji wiki hii baada ya kuumia mguu wake wa kulia katika mchezo uliokwisha kwa sare ya 1-1.

  Beki wa Chelsea, Kurt Zouma anatarajiwa kuwa nje kwa miezi sita baada ya kuumia goti PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kinda huyo ataikosa sehemu yote iliyobaki ya msimu, michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ambayo itafanyika kwenye ardhi ya nchi yake na atalazimika kupambana ili kurejea mwanzoni mwa msimu ujao.
  Zouma ameposti kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Vipimo leo vimeonyesha nimeumia ACL. Nitafanyiwa upasuaji wiki hii na nitarejea imara. Asanteni wote kwa ujumbe wenu.’ 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KART ZOUMA NJE MIEZI SITA, ATAKOSA HADI MICHUANO YA EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top