• HABARI MPYA

  Sunday, February 07, 2016

  NI DRC MABINGWA WA CHAN 2016, IVORY COAST WASHIKA NAFASI YA TATU

  JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndiyo mabingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
  Hiyo inafuatia kuifunga Mali mabao 3-0 katika fainali ya michuano ya mwaka huu Uwanja wa Amahoro, Kigali, nchini Rwanda.
  Na kwa ushindi huo, Kongo wamepatiwa dola za Kimarekani 750,000 wakati Mali wamepata dola 400,000 kwa kumaliza nafasi ya pili. Ivory Coast waliomaliza nafasi ya tatu na Guinea wa nne, kila timu imepata dola 250,000.
  Elia Meschack alifunga dakika ya 28 na 62 kabla ya Jonathan Bolingi kufunga la tatu dakika ya 73 kuifanya DRC itwae taji la pili katika fainali za nne tangu kuanzishwa kwa CHAN.
  Ikumbukwe DRC ndiyo mabingwa wa fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

  DRC wamerudia mafanikio ya mwaka 2009 walipotwaa ubingwa wa fainali za kwanza za CHAN nchini Ivory Coast

  Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Ivory Coast iliifunga mabao 2-1 Guinea na kunyakua Medali ya Shaba.
  Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na Mohamed Youla aliyejifunga dakika ya 33 na Gbagnon Anice Badie dakika ya 35, wakati la Guinea lilifungwa na Aboubacar Leo Camara dakika ya 86.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI DRC MABINGWA WA CHAN 2016, IVORY COAST WASHIKA NAFASI YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top