• HABARI MPYA

  Tuesday, February 09, 2016

  NAHODHA WA KENYA VICTOR WANYAMA NJE WIKI SITA KWA 'MIRAFU' YAKE

  KADI NYEKUNDU ZA WANYAMA 2015/16 

  Novemba 1; dhidi ya Bournemouth
  Januari 2; dhidi ya Norwich
  Februari 6; dhidi ya West Ham
  NAHODHA wa Kenya na kiungo wa Southampton ya Ligi Kuu ya England, Victor Wanyama atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita baada ya FA ya England kumfungia mechi tano kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya West.
  Hiyo ilikuwa mara ya tatu kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 kuonyeshwa kadi nyekundu msimu huu, anaongezewa mechi mbili za kukosa baada ya rafu aliyomchezea Dimitri Payet.
  Kiungo wa Southampton, Victor Wanyama akiinuka baada ya kumchezea rafu Dimitri Payet PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mkenya huyo alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Bournemouth mwezi Novemba na tena akaonyeshwa kadi mbili za njano dhidi ya Norwich mwanzoni mwa Januari.
  Inamaanisha Nahodha huyo wa Kenya, ambayo jukumu lake ni kuilinda safu ya ulinzi katika mfumo wa Saints, hataonekana uwanjani hadi kwenye mchezo wa nyumbani dhidi ya Liverpool Machi 19.
  Pia anakabiliwa na faini ya klabu ya kukatwa hadi mshahara wa wiki mbili, na kocha Ronald Koeman amesema: "Hii si kadi nyekundu ya kwanza kwake, ni ya tatu, na hiyo si nzuri. Unatakiwa kujifunza kutokana na makosa yako, hivyo nitazungumza naye juu ya hilo,"amesema.

  MECHI AMBAZO WANYAMA ATAZIKOSA 

  Februari 13 Vs Swansea (Ugenini)
  Februari 27 Vs Chelsea (Nyumbani)
  Machi 1 Vs Bournemouth (Ugenini)
  Machi 5 Vs Sunderland (Nyumbani)
  Machi 12 Vs Stoke (Ugenini)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAHODHA WA KENYA VICTOR WANYAMA NJE WIKI SITA KWA 'MIRAFU' YAKE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top