• HABARI MPYA

    Monday, February 08, 2016

    MECHAK MCHEZAJI BORA, RWANDA YATOA WA BENCHI KIKOSI CHA CHAN

    KIUNGO wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),Elia Mechak amechaguliwa Mchezaji Bora wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) iliyofikia tamati jana mjini Kigali, Rwanda.
    Mchezaji huyo wa Don Bosco ya Ligi Kuu ya DRC, jana alifunga mabao mawili wakati Kongo ikiifunga 3-0 Mali na kutwaa ubingwa wa CHAN Uwanja wa Amahoro, Kigali nchini Rwanda.
    Na kwa mabao hayo, Mechak pia amekuwa mfungaji bora wa CHAN ya 2016 kwa kufikisha mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao.

    N’Guessan Serge wa Ivory Coast ameshinda tuzo ya Bao Bora la Mashindano kutokana na bao alilofunga dhidi ya Cameroon, wakati DRC mbali na ubingwa imeshinda tuzo ya Mchezo wa Kiungwana.
    Kikosi Bora CHAN 2016 kinaundwa na kipa; Ley Matampi (DRC), mabeki; Abdoul Karim Dante (Mali), Joel Kimwaki (DRC), Cheick Ibrahim Comara (Ivory Coast), Mohamed Youla (Guinea).
    Viungo; Ibrahima Sory Sankhon (Guinea), Mechack Elia (DRC), N’Guessan Serge (Ivory Coast), Hamidou Sinayoko (Mali) na washambuliaji; Jonathan Bolingi (DRC) na Sekou Koita (Mali).
    Wchezaji wa akiba walioteuliwa ni; Badra Ali Sangare (Ivory Coast), Djigui Diarra (Mali), Lomalisa Mutambala (DRC), Heritier Luvumbu (DRC), Daouda Camara (Guinea), Aka Essis (Ivory Coast), Ernest Sugira (Rwanda), Ahmed Akaichi (Tunisia), Elvis Chisom Chikataba (Nigeria) na Christopher Katongo (Zambia).
    DRC ilitwaa ubingwa wa CHAN, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee kwa kuifunga Mali mabao 3-0 katika fainali Uwanja wa Amahoro, Kigali, nchini Rwanda.
    Na kwa ushindi huo, Kongo wamepatiwa dola za Kimarekani 750,000 wakati Mali wamepata dola 400,000 kwa kumaliza nafasi ya pili. Ivory Coast waliomaliza nafasi ya tatu na Guinea wa nne, kila timu imepata dola 250,000.
    Elia Mechack alifunga dakika ya 28 na 62 kabla ya Jonathan Bolingi kufunga la tatu dakika ya 73 kuifanya DRC itwae taji la pili katika fainali za nne tangu kuanzishwa kwa CHAN.
    Ikumbukwe DRC ndiyo mabingwa wa fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
    Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Ivory Coast iliifunga mabao 2-1 Guinea na kunyakua Medali ya Shaba.

    Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na Mohamed Youla aliyejifunga dakika ya 33 na Gbagnon Anice Badie dakika ya 35, wakati la Guinea lilifungwa na Aboubacar Leo Camara dakika ya 86.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHAK MCHEZAJI BORA, RWANDA YATOA WA BENCHI KIKOSI CHA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top