• HABARI MPYA

  Tuesday, February 09, 2016

  FURAHA YA KABILA DRC KUBEBA CHAN 2016, AWAZAWADIA MAGARI WACHEZAJI

  RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila ametimiza ahadi yake kwa kumpa kila mchezaji wa timu ya taifa gari kila moja baada ya kutwaa ubingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
  DRC walitwaa Kombe hilo Jumapili kwa kuifunga Mali mabao 3-0 katika fainali ya michuano ya mwaka huu Uwanja wa Amahoro, Kigali, nchini Rwanda na leo wachezaji wote walialikwa Ikulu mjini Kinshasa kwa pongezi na zawadi zao za magari.
  Wachezaji wa DRC wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Kabila leo Ikulu mjini Kinshasa
  Gari aina ya Jeep zikiwa viwanja vya Ikulu mjini Kinshasa leo
  Benchi la Ufundi na wachezaji wote, kila mmoja ana Jeep lake moja

  DRC ambao walipewa dola za Kimarekani 750,000 kwa kutwaa Kombe hilo, huku Mali wakipata dola 400,000 kwa kumaliza nafasi ya pili. Ivory Coast waliomaliza nafasi ya tatu na Guinea wa nne, kila timu imepata dola 250,000 walifurahi pamoja na Rais wao leo.
  Ikumbukwe DRC ndiyo mabingwa wa fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FURAHA YA KABILA DRC KUBEBA CHAN 2016, AWAZAWADIA MAGARI WACHEZAJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top