• HABARI MPYA

    Wednesday, February 10, 2016

    16 BORA KOMBE LA TFF, SIMBA NA AZAM WAPEWA RAIA WENZAO, YANGA WAPANGIWA 'WAJEDA'

    RATIBA 16 BORA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION...
    Februari 26, 2016
    Ndanda FC Vs JKT Ruvu (Nangwanda, Mtwara) 
    Coastal Union Vs Mtibwa Sugar (Mkwakwani, Tanga)
    Februari 27, 2016
    Mwadui FC Vs Rhino Rangers (Mwadui, Shinyanga) Prisons Vs Mbeya City (Sokoine, Mbeya)
    Februari 28, 2016
    Simba SC Vs Singida United (Taifa, Dar es Salaam) 
    Panone FC Vs Azam FC (Ushirika, Moshi)
    Toto African Vs Geita Gold (Kirumba, Mwanza)
    Machi 1, 2016
    Yanga SC Vs JKT Mlale (Taifa, Dar es Salaam)
    Simba SC watamenyana na Singida United 16 Bora Kombe la Azam Sports HD

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC itamenyana na Singida United katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup, wakati Yanga SC itamenyana na JKT Mlale na Azam FC itamenyana na Panone.
    Ratiba iliyotolewa leo inaonyesha kwamba mechi za 16 Bora ya Kombe la TFF zitaanza kutimua vumbi wikiendi ya Februari 26 na kufikia tamati Machi 1, mwaka huu.
    Michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64 kutoka ngazi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF nchini.
    Ijumaa tarehe 26 Februari kutachezwa michezo miwili ambapo, Ndanda FC watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    Jumamosi, Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex - Shinyanga, Jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza na mshindi kati ya Mbeya City/Wenda FC kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
    Februari 28, michezo mitatu itachezwa, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC watacheza dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto African wakicheza na wachimba madini wa Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
    Raundi hiyo itamalizika Machi 01, 2015 kwa mchezo mmoja, Yanga SC wakiwakaribisha JKT Mlale Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo, ataiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 16 BORA KOMBE LA TFF, SIMBA NA AZAM WAPEWA RAIA WENZAO, YANGA WAPANGIWA 'WAJEDA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top