• HABARI MPYA

  Monday, November 16, 2015

  MALALE ATAJA BUNDUKI ZA MAANA KUELEKEA ETHIOPIA

  Na Ali Cheupe, ZANZIBAR
  KUFUATIA kupangwa kwenye nkundi ambali linatajwa kama la kifo kwenye mashindano ya CECAFA Senior Challenji Cup nchini Ethiopia kocha msaidizi wa kikosi cha timu ya taifa Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ Malale Hamsini Keya leo ametaja bunduki zake zitakazoelekea kwenye ngarambe hizo.
  Malale ambaye amepata baraka zote za kutaja kikosi hicho kutoka kwa kocha wake mkuu Hemed Suleiman Moroko ammbaye yupo na kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ asubuhi ya leo huko uwanja wa Amaan mjini Unguja mara baada ya mazoezi ametekeleza agizo hilo.
  Kocha Malale (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari

  Wanandinga ishirini ambao wameteuliwa kwenda kupeperusha bendera ya visiwa hivyo nchini Ethiopia ni: Makipa: Mwadini Ali Mwadini (Azam) na Mohammed Abrahman (JKU).
  Walinzi: Nassor Masoud ‘Cholo’ (Stand United), Ismail Khamis (JKU), Adeyum Saleh (Coastal Union), Mwinyi Haji Mngwali (Yanga), Agrey Morris (Azam), Issa Haidar (JKU), Said Mussa ‘Udindi’ (Mafunzo), Nadir Haroub ‘Canavaro’ (Yanga).
  Viungo: Said Makapu (Yanga), Awadh Juma Issa (Simba), Mudathir Yahya (Azam), Omar Juma (Chipukizi), Suleiman Kassim ‘Selembe’ (Stand United), Khamis Mcha (Azam), Mohammed Abrahman (Mafunzo).
  Washambuliaji: Matheo Anthon Simon (Yanga), Ibrahim Hilika (Zimamoto) na Ame Ali zungu (Azam).
  Akizungumza mara baada ya kutaja kikosi hicho kocha huyo amesema kiukweli kundi ambalo Zanzibar wamepangwa siyo rahisi ikizingatiwa kuwa hata bingwa mtetezi wa kombe hilo Harambee Stars ya Kenya wapo pamoja.
  Kwenye mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Novemba 21 nchini Ethiopia, Zanzibar Heroes wapo kundi B sambamba na Kenya, Uganda na Burundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALALE ATAJA BUNDUKI ZA MAANA KUELEKEA ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top