• HABARI MPYA

    Monday, November 16, 2015

    RWANDA YAPANGWA KUNDI LA KIFO FAINALI ZA CHAN 2016 KIGALI

    Na Hamadi Harakaze, KIGALI
    WENYEJI Rwanda wamepangwa kundi la kifo katika michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), wakiwekwa pamoja na vigogo Ivory Coast, Morocco na Gabon katika Kundi A.
    Katika droo iliyopangwa jana mjini Kigali, Rwanda - Nigeria imepangwa Kundi C pamoja na Tunisia, Niger na Guinea.
    Uganda walioitoa Tanzania kwenye hatua za awali za michuano hiyo, wamepangwa Kudi D pamoja na Zimbabwe, Mali na Zambia, wakati Kundi B lina timu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ethiopia, Cameroun na Ethiopia.

    Mabingwa watetezi, Libya, waliofunga Ghana kwa penalti 4-3 katika fainali zilizopita, hawakufuzu safari hii.

    MAKUNDI: 
    KUNDI A: Rwanda. Gabon, Ivory Coast, Morocco
    KUNDI B: DRC, Ethiopia, Cameroon, Ethiopia
    KUNDI C: Tunisia, Nigeria, Niger, Guinea
    KUNDI D: Zimbabwe, Mali, Uganda, Zambia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RWANDA YAPANGWA KUNDI LA KIFO FAINALI ZA CHAN 2016 KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top