• HABARI MPYA

    Tuesday, November 24, 2015

    AZAM FC WAANZA 'MAKAMUZI' LEO KWA AJILI YA SIMBA SC

    VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC leo wanatarajiwa kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba SC mwezi ujao.
    Benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu Stewart Hall, liliwapa mapumziko ya wiki tatu wachezaji mara baada ya kumalizika kwa mechi ya raundi ya tisa ya ligi dhidi ya Toto Africans, iliyoisha kwa Azam FC kushinda mabao 5-0.
    Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Idd, amesema mazoezi hayo yatahusisha wachezaji takribani 10 wa timu kubwa watakaochanganyika na timu ya vijana ya timu hiyo.
    Azam FC kwenye mazoezi hayo, itawakosa wachezaji takribani 12 waliokuwa timu za Taifa za Tanzania Bara, Zanzibar, Rwanda, Burundi na Kenya, wakishiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Ethiopia hadi Desemba 6, mwaka huu.
    Kikosi cha Azam FC kinachosumbua katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

    “Timu itaanza na mazoezi mepesi kesho asubuhi, ikiwasubiria nyota waliokuwa timu za Taifa, kutokana na upungufu wa wachezaji wengi wa timu kubwa, watachanganyika na wachezaji wa timu ya vijana,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WAANZA 'MAKAMUZI' LEO KWA AJILI YA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top