• HABARI MPYA

    Friday, November 20, 2015

    STARS YAWASILI SALAMA ADDIS TAYARI KWA CHALLENGE 2015

    KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ tayari kimewasili Addis Ababa nchini Ethiopia leo alfajiri kikiwa na wachezaji 18 pamoja na vinogozi tayari kwa mashindano ya Kombe la Chalenji yatakayoanza kutimua vumbi kesho Jumamosi nchini humo.
    Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha mkuu Abdallah Kibadeni, akisaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, imepangwa katika kundi A, ikiwa na wenyeji timu ya taifa ya Ethiopia, Rwanda, pamoja na Somalia.
    Kocha wa Taifa Stars, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden'

    Wachezaji waliosafiri na timu hiyo ni magolikipa Ally Mustafa na Aishi Manula, walinzi Shomari Kapombe, Kessy Radmahani, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Ishaka, Salim Mbonde na Kelvin Yondani.
    Wengine ni viungo Himid Mao, Salum Abubakar, Jonas Mkude, Salum Telela na Said Ndemla, huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Malimi Busungu, Elias Maguri, Saimon Msuva, Deus Kaseke na nahodha John Bocco.
    Stars itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Somalia siku ya Jumapili katika uwanja wa Addis Ababa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS YAWASILI SALAMA ADDIS TAYARI KWA CHALLENGE 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top