• HABARI MPYA

    Sunday, November 22, 2015

    BOBBY AMTAMBIA MICHO; HARAMBEE STARS YAITANDIKA THE CRANES 2-0

    MATOKEO NA RATIBA CHALLENGE 2015
    Novemba 21, 2015
    Burundi 1-0 Zanzibar 
    Ethiopia 0-1 Rwanda
    Novemba 22, 2015
    Somalia 4-0 Tanzania 
    Kenya 2-0 Uganda 
    Novemba 23, 2015
    Sudan Kusini v Djbouti 
    Sudan v Malawi
    Novemba 24, 2015
    Zanzibar Vs Uganda 
    Rwanda Vs Tanzania 
    Novemba 25, 2015
    Kenya Vs Burundi 
    Somalia Vs Ethiopia 
    Malawi Vs Djibouti
    Sudan Kusini Vs Sudan
    Novemba 27, 2015
    Rwanda Vs Somalia
    Zanzibar Vs Kenya
    Sudan Kusini Vs Malawi
    Djibouti Vs Sudan
    Novemba 28, 2015
    Uganda Vs Burundi 
    Tanzania Vs Ethiopia
    Wachezaji wa Harambee Stars wakifurahia ushindi wao leo

    MABINGWA watetezi, Kenya, wameanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuifunga Uganda, The Cranes 2-0 leo Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa Ethiopia katika mchezo wa Kundi B.
    Shukrani kwao, washambuliaji Jacob Keli wa Nkana United na Michael Olunga wa Gor Mahia walioifungia mabao hayo timu ya Mscotland, Bobby Williamson dhidi ya kikosi cha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’.
    Ikumbukwe Bobby alikuwa kocha wa Uganda kabla ya kuondoka na FUFA kumuajiri Micho – hivyo leo amekuwa mwenye furaha kuifunga timu yake ya zamani.
    Katika mchezo wa kwanza, Tanzania Bara au Kilimanjaro Stars imeanza vyema pia baada ya kuifunga Somalia mabao 4-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia.
    Matokeo hayo, yanaifanya Kili Stars inayofundishwa na mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ianzie kileleni mwa Kundi A ikiwashusha Rwanda walioifunga Ethiopia 1-0 jana. 
    Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ amefunga mabao mawili katika ushindi huo, moja kwa penalti dakika ya 12 baada ya beki wa kulia, Shomary Kapombe kuangushwa na lingine dakika ya 54. 
    Mshambuliaji pacha wake leo, Elias Maguri naye akafunga mabao mawili dakika ya 17 na 66 kukamilisha kipigo kama ambacho Barcelona iliipa Real Madrid jana katika La Liga Uwanja wa Bernabeu.
    Michuano hiyo itaendelea kesho kwa michezo ya Kundi C, baina ya Sudan Kusini na Djbouti na Sudan dhidi ya Malawi baadaye mjini Awassa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOBBY AMTAMBIA MICHO; HARAMBEE STARS YAITANDIKA THE CRANES 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top