• HABARI MPYA

    Wednesday, November 18, 2015

    BRAHIMI ASEMA HIMID, MAGURI, ULIMWENGU NA SAMATTA NI VIWANGO VYA ULAYA

    Na Mahmoud Zubeiry, BLIDA
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Algeria, Yacine Brahimi amesema Tanzania ina wachezaji wazuri wanaostahili kucheza Ulaya kama Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, Elias Maguri na Himid Mao.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana baada ya mchezo ambao Algeria iliifunga Tanzania mabao 7-0 Uwanja wa wa Mustapha Tchaker mjini Blida, Brahimi alisema Tanzania wana timu nzuri.
    Alisema Algeria ilitumia uzoefu wake kuifunga Tanzania, lakini bado haipotezi ukweli walikutana na wapinzani wazuri.
    “Waliendelea kutengeneza nafasi hata baada ya kuwa nyuma kwa mabao 7-0. Hiyo ni timu nzuri, haikufa moyo uwanjani. Mabao yote walifungwa kwa makosa ya kawaida ya mchezo,”alisema.
    Yacine Brahimi akimtoka Shomary Kapombe jana Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida

    “Nadhani kocha atarekebisha mfumo na makosa ilia pate matokeo mazuri baadaye,”aliongeza.
    Lakini Brahimi anayechezea FC Porto ya Ureno alionekana kuvutiwa mno na Samatta na akasema anaamini atakuwa mmoja wa wachezaji bora wa Kiafrika baadaye.
    “Samatta, hata yule namba 11 (Ulimwengu), namba 15 (Elias Maguri) na saba (Himid) ni wachezaji wazuri ambao wanastahili kucheza Ulaya,” alisema Brahimi baada ya kuulizwa ni wachezaji gani wa Tanzania wana uwezo wa kucheza Ulaya.
    Mabao ya Algeria jana yalifungwa na Yacine Brahimi, Ghoulam Faouzi, Mahrez Ryad, Islam Slimani, Ghezzal Faouzi, Carl Medjani na Ghezzal Rachid – na kwa matokeo hayo Taifa Stars inatolewa kwa jumla ya mabao 9-2, baada ya awali kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbweha hao wa Jangwani katika mechi ya kwanza iliyochezwa Jumamosi mjini Dar es Salaam.
    Mabao yote ya Algeria Dar es Salaam yalifungwa na Slimani Islam wakati ya Stars yalifungwa na Maguri na Samatta
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRAHIMI ASEMA HIMID, MAGURI, ULIMWENGU NA SAMATTA NI VIWANGO VYA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top